BREAKING NEWS

VIDEO ZA AFYA

DAWA ZETU

USHAURI WA AFYA

Jumatano, 2 Desemba 2015

ISOME MAKALA HII ILI UZITAMBUE DALILI ZA MIMBA CHANGA



Habari za leo mpenzi msomaji wa makala zetu, leo tunapenda kugusia kwa kiasi kidogo kuhusu dalili za mimba changa. Hili somo tumeamua kulileta baada ya wasomaji wetu wengi kuendelea kutuuliza maswali kuhusu namna mwanamke anavyoweza kugundua kuwa ni mjamzito hasa kwa akinadada ambao ndiyo mara yao ya kwanza kuwa katika hali hiyo.

Zifuatazo ni baadhi ya dalili ya mimba changa:
KWANZA. Mabadiliko katika siku zako(spotting). Unaweza kupata mimba na ukaendelea kuona damu mwezi huo. Hii hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza katika kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa katika ukuta huu tayari kulisha kiumbe huachia damu kidogo ambazo mwanamke anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida. Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani kiwango cha siku za damu hubadilika.

PILI. Kuongezeka ukubwa na kupata maumivu kwenye maziwa(chuchu). Hii inasababishwa na kuongezeka kwa homoni za estrogen pale unakuwa umeshika mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.

TATU. Kichefuchefu na kutapika. Hali hii huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi unapotoka kulala. Na hii ni kwa sababu ya homoni za progesteron ambazo husababisha kupungua nguvu kwa msuli wa mrija wa chakula au koromeo.

NNE. Uchovu na usingizi usiokuwa wa kawaida na bila sababu. Hali hii husababishwa na ongezeko la homoni ya progesteron na mama utajikuta unapata usingizi kila mara. Hali hii huisha unapoanza mwezi wa nne wa mimba.

TANO. Kusumbuliwa na harufu mbalimbali. Hii hutokea hasa unapopata mimba ya kwanza utachukia harufu ya baadhi ya vyakula na vinywaji mbalimbali. Wakati mwingine hata harufu za baadhi ya watu zinaweza kukukera. Hapa kidogo panachekesha kwani baadhi ya akinamama huchukia hata harufu ya wapenzi au waume zao.

SITA. Kujaa gesi tumboni. Utaona baadhi ya nguo zako zinakubana zaidi sehemu ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya homoni nyingi mwilini zinakufanya kujisikia tumbo kujaa.

SABA. Kukojoa mara kwa mara. Hii hutokana na kuwa na damu nyingi mwilini ambayo huongezwa na homoni za ujauzito makusudi kutoa lishe ya kutosha kwa mama na kiumbe kilichomo tumboni. Kikemia ukiwa na damu nyingi mwilini utakojoa sana. Pili utajisikia kwenda sana haja ndogo mara nyingi pale kiumbe kitapoongezeka na kubana kibofu cha mkojo.

NANE. Kuongezeka kwa joto la mwili. Kwa akinamama ambao hupima joto lao kwa njia ya uzazi wa mpango, watagundua kuwa joto limepanda kwa muda wa wiki mbili au mbili na nusu mfululizo.

TISA. Kutoona siku zako za hedhi kabisa. Kwa akinamama ambao siku zao hazibadiliki au huenda vizuri yawezekana wakagundua pale wanapokosea siku na pengine kukimbilia hospitali. Hata hivyo kwa wale ambao siku zao hubadilika sana wataona ni kawaida ila kama ameshika mimba ataona mchanganyiko wa kichefuchefu, uchovu, kusinzia pamoja na kukojoa mara kwa mara.

KUMI. Kupima mkojo kwa kutumia kipimo cha karatasi ngumu. Pharmacy nyingi huuza vipimo ambavyo ukivichovya kwenye mkojo wako huweza kugundua homoni za mimba kwenye mkojo. Hii unaweza kupima mwenyewe ukiwa nyumbani au hata kazini. Kipimo hiki ukikichovya kwenye mkojo kama karatasi inavyoelekea utaona mistari baada ya dakika moja inajitokeza upande wa chini, ikitokea mistari miwili basi utakuwa una mimba na ukitokea mmoja itakuwa hauna mimba. Lakini kipimo hiki huwa kina changamoto zake kwa baadhi ya akinamama ambao kulingana na matatizo ya kiwango cha homoni mwilini hakitaweza kuonyesha majibu mpaka wapitishe wiki moja bila kuona siku zao.

Pamoja na dalili hizo hapo juu, ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu zaidi kutoka kwa daktari aliyepo karibu na wewe.

Maoni 9 :

  1. Naomba kuuliza swali Mimi nilikuwa natumia uzazi wa mpango kwa sasa nimeacha na huu ni mwezi wa Tatu toka niache mwezi wa kwanza niiingia kwenye cku vizuri baada ya kuacha uzazi wa mpango mwezi wa Pili sijaingia kabisa ila sioni dalili zozote za mimba hata nikitumia pregnant test inaonesha negative msaada wenu nifanyaje wapendwa.

    JibuFuta
  2. Mimi nilikuwa natumia uzazi wa mpango kwa sasa nimeacha nataka kupata mimba lakini sipati nambeni msaada

    JibuFuta
  3. Muone doctor kwa msaada zaid

    JibuFuta
  4. Sina mimba Ila Nina mwex wa4 xjabreed, naomb uxhaury

    JibuFuta
  5. Na tumbo huwa yauma hapo wiki zamwanzo

    JibuFuta
  6. Pamoja na dalili za maziwa kuuma vipi kuwasha na damu kutoka matone matone yani unakuta kila siku ni tone labda asubuhi tu au usiku

    JibuFuta
  7. Jamani mm maziwa yangu yamejaa ns yanauma lakini ninakula sana,nilitakiwa kublidi trehe 6 lkini adi sasa ni tarehe 12 na nilpma baada ya wiki moja baada yakugundua nimefnya siku 11 nikakuta Sina mimba hili nitatizo gn tenaa

    JibuFuta
  8. Mimi kichwa kinawaka moto yaan joto huku mwilini baridi pia mwili kuchoka na kuuma,,,,siku zangu sizioni,,,
    Naomba ushaur

    JibuFuta

 
Copyright © 2013 NGALAWA HEALTH CONSULTANT
Powered by WordPress24x7