Siku mwanadamu atakapo kuja kugundua kuwa siri ya mafanikio yake yako mikononi mwake basi ndio utakuwa mwisho wa umaskini wake.
Tutakuwa tunajiuliza maswali mengi juu ya umaskini na
utajili. Niwakati gani unamwita mtu tajiri na mwingine unamwita maskini?
Hii maana yake huwezi kutambua kuwa fulani ni tajili na fulani ni
maskini pasipo kuwalinganisha kati yao. Ikitokea watu wote wakawa na
kipato kimoja na maisha sawa apo huwezi tambua yupi maskini wala tajili.
Apo ndio utagundua ili utofautishe jambo fulani eidha kwa ubora au kwa
uzuri lazima uwe na chakulinganisha nacho.
Sasa ndio maana kila mtu anatofautiana katika njia za
utafutaji wake na hii kila mtu anamlango wake alio fungua maishani mwake
ila inatofautiana kwa kiasi kikubwa mpaka kupelekea kuwa na makundi ya
watu maskini na watu tajili.
Nataka nikwambie kitu ndugu yangu kuwa,iwe unataka kuwa
maskini au tajili funguo ziko mikononi mwako kuweza kuufungua mlango
sahihi wa maisha yako. Na utambue kuwa hakuna mtu mwenye funguo za
mwenzake kila mtu ana zake.
Sasa jiulize ni mlango gani unapaswa kufungua ili ufanikiwe?
Wakati naanza kujiajili nilifikilia mambo mengi sana kuwa
ni mlango gani nifungue ikiwa funguo ninazo mimi mwenyewe? Ila nilikaa
chini na kutafakari kuwa hakuna mtu awezaye kuja kunibadilishia maisha
yangu ila ni mimi mwenyewe kuweza kuamua kuchagua mlango wa kufungu.
Milango ipo mingi ila mimi mlango sahii kwangu ni mlango wa
ujasiliamali. Siosiri ndugu yangu nayafurahia maisha haya,maana hakuna
anaye nibana sipangiwi ratiba na mtu,naifanya kazi yangu nikiwa sehemu
yoyote ata niwe nyumbani au niwe safarini naifanya tu.
Na siri ya mafanikio hayo ni toka nilopogundua kuwa
nikiweza kutumia MUDA wangu vizuri nitafanikiwa, ikabidi niamue
kuwekeza sasa kwa WATU hii inanisaidia sana maana JUHUDI na maarifa
ninayotumia yanazidi kuongeza kipato changu kila siku.
Lazima utambue kuwa hakuna kazi ngumu kama kuamisha pesa ya
Mtu kutoka mfukoni mwake na kuja mfukoni mwako,ila ukiweza jua mbinu ya
kufanya hivyo basi nirahisi sana. Vitu hivi MUDA,WATU na JUHUDI
vimekuwa funguo ktk maisha yangu.
Sasa basi swali la kujiuliza ni,Je wewe unaitaji kufungua
mlango wako wa mafanikio? Kama jibu ni NDIO basi ungana nami
nikufundishe mbinu sahii za kujiajili kwa kutumia MUDA,WATU NA JITIHADA
kama fungu za maisha yako kwa kutumia muda wa ziada.
Tambua kuwa msukumo wako unatakiwa kutoka moyoni
mwako,hakuna mtu awezaye kuja na kufikilia badala yako bali wewe ndio
muamuzi wa maisha yako,FUNGUO ZIKO MIKONONI MWAKO IVYO NI MAAMUZI YAKO
KUFUNGUA MLANGO SAHIHI
Chapisha Maoni