Jumatano, 2 Desemba 2015
HIZI NDIO NJIA ZA KUJITOA KWENYE KIFUNGO CHA UMASKINI
Habari za leo ndugu msomaji wangu. Nisiku nyingine tena tunakutana apa kwa lengo la kuelimishana na kuabalishana ili tuweze kuakikisha tunamtokomeza adui yetu mkubwa UMASKINI. Katika dunia ya leotumekuwa tukishindwa kufikia malengo yetu kutokana na sababu mbali mbali zinazo tukabili katika maisha yetu ya kila siku. Sababu ni nyingi ila kwa leo sitazizungumzia bali ninapenda kwa nafasi ya pekee niweze kuzungumzia njia ambazo ndio muongozo katika maisha yetu ili tuweze kukabiliana na changamoto zinazo tukumba kilahisi. Ukiwa kama kijana unaye taka kuleta mabadiliko katika maisha yako inatakiwa mambo yafuatayo uyazingatie sana:
1. AMINI UNAWEZA.
Kati ya mambo makubwa yanayotukwamisha katika kufikia ndoto zetu ni kuhisi kuwa hatuwezi kufanya jambo fulani. Ondoa katika fikra izo maana pindi unapo hofu kuwa huwezi kumbuka unateketeza ndoto zako. Jiamini kuwa unaweza,hakuna mtu anaye weza kuja kubadili maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe.
2. ONDOA MAMBO YASIO KUFAA KATIKA MAISHA YAKO.
Kama unahisi kunamambo ambayo sio ya msingi achana nayo,huwezi kuwana gorofa bila kukubali kufuta mawazo ya nyumba ya kawaida akilini mwako. Ukiwa unataka mabadiliko badili mtazamo wako uondokane na mambo yanayokupotezea muda.
3. FANYA KAZI KWA BIDII.
Ndoto za maisha huwa hazitokei kama miujiza,bali ukutaka utoke jasho na ujitoe kwa dhati. Vikwazo utoweka endapo ukijitoa kwa moyo katika kupambana nazo ili kuzielekea ndoto zetu na malengo yetu,na kila uamkapo asubuhi amka ukiwaza kupambana.
4. JISIMAMIE MWENYEWE.
Huwezi kumlazimisha mtu akueshimu, lakini huwezi kukubali mtu hasikueshimu. Kama ukiamua kujishusha ili kuepuka shari,basi utashambuliwa na kila mtu. Simama na upambane husikubali mtu au kitu chochote kiwe kikwazo kwako katika kuyatafuta maendeleo.
5. SAHAU YALIOPITA.
Husikae na kuwaza vikwazo na misukosuko ya nyuma, husiwe mtumwa wa yalio pita,hacha yapite na anza maisha mapya. Ndoto yako ndio dira yako.
6. HACHANA NA MAUSIANO YASIOFAA.
Kuwa na mtu katika maisha ya nyuma,haimaanishi kuwa ndio utakaye kuwa nae katika maisha ya baadae. Kumkumbuka mtu wako wa awali haimaanishi kuwa unamuitaji kwa sasa,kumkosa mtu wa awali ni sehemu bola ya wewe kusonga mbele.
7.MSHUKURU MUNGU WALAU KWA ICHO ULICHO NACHO.
Ataka kama vikwazo ni vingi ,shukulu kwa yale mema ulionayo na tabasamu. Jisemee moyoni 'sitashindwa,bali nitashinda'
8. TENGA MUDA KIDOGO KILA SIKU WA KUYAFURAIA MAISHA YAKO.
Pale tu unapoa kaa chini peke yako nakuanza kuyatafakari maisha yako,kwa mapungufu yako,vikwazo na uwezo wako katika kupambana,kisha tufurahie uwezo wetu.
9. KUBALI KUJIFUNZA ILI UENDANE NA WAKATI
Mbegu ya mafanikio imepandwa ndani ya anguko lako la nyuma. Hadithi yako nzuri itatoka katika mapambano ya awali,simama imara na songa mbele. Ata majira ya baridi hubadilika nakuwa ya vuli. Ivyo ata usiku hubadilika nakuwa mchana.
10. FURAHIA ULIPO SASA.
Wakati mwingi tunaweza kuwa bize tukitizama mbele,ivyo hatupati muda wakufuraia maisha tulio nayo. Unaweza kuwa hujafikia pale ulipo palenga ila walau umefikia sehemu fulani ambayo ni tofauti na awali.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Chapisha Maoni